Loading...
 

Kushirikisha Klabu za Nje

 

 

Kama unaendesha shirika lisilo la kiserikali, huduma za kijamii, au klabu iliyopo yenye shughuli ambazo zinaendanan na kanunui za msingi za Agora Speakers International, unaweza ukawapatia wanachama wako na faida za ziada za kujiunga jamii ya Agora.

Faida za Ushirikiano

Kwa kushirikiana na Agora, unawapatia wanachama wako uanachama kamili wa Agora na ufikivu wa dunani kote wa jamii ya Agora - ikiwemo nyenzo za kielemu, mashindano ya kimataifa, jukwaa letu la kimataifa, mawasiliano, na vifaa vya usimamizi, kupata mawasiliano na nafasi ya kupata ushauri, nk. Wataweza kuhudhuria mikutano kwenye klabu yoyote ya Agora duniani kote, kushiriki kwenye matukio yote ya Agora, nk.

  • Kama shirika lako lisilo la kiserikali, huduma ya kijamii, au klabu uliopo mnakutana mara kwa mara, njia rahisi ni kubadilisha baadhi ya hii mikutano iwe na mtindo wa mikutano ya Agora. Kwa mfano, kama klabu yako mnakuana kila wiki, unaweza kuamua kuwa mmoja wa mkutano wa kila mwezi, uwe "mkutano wa Agora". Kwa njia hii, inakuwa kama "klabu ndani ya klabu".
  • Chaguo lini ni kuendeleza kidogo shughuli mlizonazo na "mwendelezo wa mkutano wa Agora". Kwahiyo, kwa mfano, kama mnakutana mara kwa mara kuchangisha fedha, pale shughuli hiyo itakapoisha, unaweza mkawa na mkutano wa Agora.

Ushirikiano unawekwa wazi kwa umma - wote Agora Speakers International na shirika lako litatangaza ushirikiano kwa kutoa habari ya pamoja kwenye muundo sanifu.

Mahitaji

Bila kujali hali ilivyo, kipengele cha Agora cha shughuli zenu lazima kifanye kazi kikamilifu kama klabu ya Umma ya Agora club. Hii inamaanisha:

  • Inahitaji kutii miongozo yote ya Agora ya klabu, ikiwemo kuwa na jina linalofaa, namba ya klabu, na seti ya maofisa wa klabu ambao wamechaguliwa.
  • Wanachama bado wanatakiwa kujiunga kwenye jukwaa la mtandaoni. Tunaweza kuingiza wanachama kwa ujumla kutoka kwenye orodha ya CSV, au wanaweza kujiunga kwa kawaida.
  • Mwendelezo wa klabu zote utaorodheshwa kama Klabu za Agora zilizokaribishwa kwenye jukwaa letu. Unaweza ukatoa ufafanuzi mfupi wa shirika lako, na itajumuishwa kwenye maelezo ya klabu. Lakini, mikutano iliyopangwa tu ambayo inafuata muundo wa Agora itatangazwa.
  • Mikutano yote ya aina ya Agora inatakiwa kuendeshwa kama Klabu za Umma za Wazi: Watatakiwa kukubali wageni, wanachama wengine wa Agora, na ambao wanaweza kuwa wanachama wapya wanaotaka kujiandikisha.
  • Wanachama wapya wataweza kujiunga tu kwa ajili ya mikutano ya aina ya Agora. Kwa maneno mengine, mahudhurio ya vipindi vya aina ya Agora haitohitaji uanachama wa shirika lingine lolote (hakika, japokuwa kwenye mikutano ya aina ya Agora, klabu zinaweza zikatangaza vipengele vingine pia).
  • Mahudhurio ya kipengele cha Agora hakiwezi kuhitaji matendo mengine yeyote ya shirika kuu.
  • Watu ambao wanataka kujiunga na kipengele cha Agora tu cha shughuli zenu wanatakiwa wachaguliwe kama maofisa.

 


Contributors to this page: agora and zahra.ak .
Page last modified on Monday August 30, 2021 01:43:41 CEST by agora.